March 16, 2018




Na Mwandishi Wetu, Port Said
Kaimu Rais wa Simba, Salim Try Again ndiye anaongoza mapambano ya kikosi cha Simba mjini hapa akishirikiana na viongozi wengine wa kamati ya ufundi.


Simba imeanza mazoezi ya usiku kuhakikisha inazoea hali ya hewa ya kiasi cha baridi kilicho katika mji wa Port Said nchini Misri.

Kaimu huyo rais wa Simba amekuwa bega kwa bega na kikosi hicho ambacho tayari kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Al Masry kesho.

Try Again amekuwa akishirikiana kwa karibu na kiongozi mwingine mkongwe wa Simba, Muslye Al Rawah ambaye alitangulia kufanya maandalizi. Viongozi hao wamekuwa muda wote mazoezini na kambini kilipofikia kikosi hicho wakihakikisha kuanzia mazoezi, kula, mpangilio wa nidhamu na kila kitu kinakwenda sawia.

Wachezaji na makocha wa Simba wamekuwa katika hali sahihi ya usalama na amani jambo ambalo viongozi hao wamekuwa wanalitaka ili kuwapa nafasi ya kucheza mpira kesho kwa uhakika.

Kikosi hicho kimekuwa kikiendelea na maandalizi yake kwa uhakika kabisa kutokana na kila kitu kuwa katika mpangilio na viongozi kushirikiana kwa ukaribu.

Kiongozi mwingine wa Simba ambaye amekuwa akionekana karibu na viongozi hao kuendelea na maandalizi ni Said Tulli ambaye ni kati ya wajumbe wa kamati ya utendaji.

Katika mechi ya kwanza mjini Dar es Salaam, Simba ilipata sare ya mabao 2-2 ambayo inaonekana pia kuwapa presha hata Al Masry ambao wamejichimbia pia wakiendelea na mazoezi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic