Na Mwandishi Wetu, Port Said
Simba imeanza mazoezi ya usiku kuhakikisha inazoea hali ya hewa ya kiasi cha baridi kilicho katika mji wa Port Said nchini Misri.
Simba imeanza mazoezi ya usiku kuhakikisha inazoea hali ya hewa ya kiasi cha baridi kilicho katika mji wa Port Said nchini Misri.
Jana usiku kikosi hicho kilifanya mazoezi yake ya kwanza kwenye uwanja ulio katikati ya mji huo ikiwa ni kuhakikisha inazoea ubaridi unaoongezeka hata nyakati za usiku.
Simba iko hapa Port Said kuivaa Al Masry katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Port Said. Mechi ya kwanza iliisha kwa Simba kupata sare ya bao 2-2.
Wachezaji wa Simba walionekana kuwa na ari wakati wa mazoezi na walikuwa wakichangamka kadiri muda unavyosonga mbele tofauti na walivyoanza mazoezi kutokana na hali ya ubaridi.
Kwa mujibu ya wenyeji kwa kuwa wenyewe wana uzoefu na hali ya hewa wanaona baridi si kali lakini kwa wageni wanalalamika..







0 COMMENTS:
Post a Comment