Mzunguko wa 20 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara
unaendelea kesho Jumamosi Machi 3, 2018 kwa kuchezwa mechi nne.
Njombe Mji watakuwa nyumbani Uwanja wa Sabasaba kucheza na
Ruvu Shooting mchezo utakaochezwa saa 8 mchana, wakati Kagera Sugar wao watakuwa
nyumbani Uwanja wa Kaitaba kuwakaribisha Majimaji ya Songea mchezo utakaochezwa
saa 10 jioni.
Mechi nyingine Tanzania Prisons ya Mbeya watakuwa nyumbani
Uwanja wa Sokoine kucheza dhidi ya Mbao FC ya Mwanza saa 10 jioni, Azam FC
watakuwa Azam Complex ikiwakaribisha Singida United saa 1 jioni.
(k)
ReplyDelete