Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inatarajia kucheza
michezo miwili ya kirafiki mwezi huu wa Machi kwenye tarehe za kalenda ya FIFA.
Taifa Stars itakuwa ugenini nchini Algeria Machi 22, 2018
kucheza dhidi ya Algeria kabla ya kucheza na DR Congo Machi 27, 2018 Uwanja wa
Taifa Dar es Salaam, Tanzania.
Tayari mechi hizo zimethibitishwa na pande zote mbili
kuchezwa katika tarehe hizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment