Na George Mganga
Kikosi cha Ruvu Shooting kimekubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Njombe Mji FC katika mchezo wa ligi uliochezwa mchana wa leo kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Katika mchezo huo, Njombe Mji ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Ditram Nchimbi katika dakika ya 27, na mpira uliendelea mpaka kwenye dakika ya 27, Baraka Mtuwi akaisawazishia Ruvu Shooting.
Bao la Zahir liliweza kudumu mpaka kipindi cha mapumziko ambapo mchezo ulikuwa sare ya mabao 1-1.
Kipindi cha pili kilianza na baadaye kuleta neema kwa Njombe Mji FC, ambapo katika dakika ya56, Mwaisondola aliifungia Njombe Mji bao la pili na kufanya mchezo umalizike kwa idadi ya mabao 2-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment