March 2, 2018



Na George Mganga
 
Simba imezidi kuipa unafuu Yanga katika harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kwenda sare ya mabao 3-3 dhidi ya Stand United

Walikuwa ni Simba walioanza kuliona lango la Stand katika dakika ya 6 ya mchezo kupitia kwa Ludit Mavugo, na baadaye dakika ya 26  Asante kwasi akafunga bao la pili na kuufanya mchezo kuwa 2-0.

Mambo yalianza kwenda kinyume kwenye dakika ya 36 baada ya Tariq kuifungia Stand bao la kwanza na baadaye kwenye dakika ya 41, Lulambo akaisawazishia Simba kwa njia ya kona iliyoingia kimiani moja kwa moja na kufanya dakika 45 za kwanza ziende kwa sare ya 2-2.

Kipindi cha pili kilianza vema upande wa Simba ambapo katika dakika ya 61, Nicholous Gyan alicheka na nyavu za Stand kwa kufunga bao la pili, lakini tena kwenye dakika ya 67, Bigirimana aliiswazishia Stand

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Simba SC 3-3 Stand United.

Kwa matokeo haya sasa Simba imefikisha alama 46, tofauti kwa alama 6 na Yanga iliyo na pionti 40.

3 COMMENTS:

  1. Pointi 6 ni mechi 2 tu za Yanga kushinda na Simba kushindwa basi hadithi inarudi ileile ya miaka ya nyuma. Wachezaji Simba acheni kudharau mechi hizi. Leo Stand walishalala

    ReplyDelete
  2. kwani Yanga ana uhakika gani wa kushinda mechi zote alizosalia?.....Benchi hili la ufundi wa Simba si la wakati ule wa kocha Omog.Na hata ukifuatilia utaona Simba inazidi kubadilika na kucheza mpira unaoeleweka kwa sababu wanatengeneza nafasi na wanazitendea haki.Mie sio mtabiri lakini naamini mwisho wa ligi Simba ni bingwa

    ReplyDelete
  3. Bahati mbaya wewe mwandishi habari zako sijui unazitoaga wapi. Juzi uliandika Ndanda walipata bao la kufutia machozi dk 83 wakati ilikuwa dk ya 46.Leo unatuambia Mavugo ndiye aliyeanza kuifungia Simba usiandike usichokijua

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic