March 19, 2018


Na George Mganga
 
Mshambuliaji Mtanzania, Rashid Mandawa anayeichezea klabu ya BDF XI ya Botswana,ameongezwa kwenye orodha ya wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

Stars inajiandaa kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Algeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Taifa Stars itaanza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Algeria Machi 22 2018, kabla ya kuikaribisha nyumbani timu ya taifa ya Kongo, Machi 27 2018.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga, awali aliita kikosi chenye jumla ya wachezaji 23 lakini baadhi wamepunguzwa kutokana na sababu mbalimbali.

Wachezaji walioitwa hapo mwanzo na sasa wameondolewa ni: Thomas Ulimwengu, Said Ndemla, Farid Mussa, Hamis Abdallah na John Bocco.

Walioongezwa na kufanya idadi ya wachezaji ndani ya kikosi hicho kuwa 21 ni: Himid Mao, Rashid Mandawa pamoja na  Shaaban Idd.

Kikosi hicho kitaondoka hapa nchini kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kirafiki utakaopigwa Mach 22 2018.


1 COMMENTS:

  1. Ubabaishaji mtupu. Bado tunasafari ndefu. Mayanga amekuwa kocha wa timu ya Taifa kwa kipindi sasa lakini inaonesha hana takwimu sasa za wachezaji kiasi cha kumpelekea kuchagua wachezaji kwa kubahatisha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic