March 24, 2018



Imeripotiwa kuwa klabu ya Manchester United inatajwa kumnyatia Mshambuliaji nyota wa Kibrazil, Nemyar Junior endapo ataihama PSG ya Ufaransa. Real Madrid nao wanamuhitaji mchezaji huyo. Mundo Deportive (Spain). 

Jarida la The Mirror limeandika kuwa Mshambuliaji Gareth Bale, ataikacha klabu yake ya Real Madrid na kutimkia Manchester United endapo Kocha Zinedine Zidane ataendelea kusalia kuifundisha timu hiyo. Kocha wa timu ya taifa ya Wales, Ryan Giggs amemshauri Bale kuendelea kusalia Madrid kuliko kwenda Manchester United. (Express)

Manchester City na United zote zinaiwinda saini ya beki wa kati wa Bayern Munich, Jerome Boateng (29). (The Sun).

Manchester United wamezidi kuwa kutajwa zaidi katika tetesi za usajili leo, ambapo inadaiwa wameshaweka kitita cha paundi milioni 40 mezani kumwania mchezaji, Winga wa Kibrazil kutoka Bayern Munich anayeichezea Juventus kwa mkopo, Douglas Costa.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic