March 19, 2018


Kikosi cha Taifa Stars kimeondoka mchana wa leo kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa kirafiki utakaochezwa Machi 22 2018.

Wakati kikosi hicho kikisafiri leo, Mshambuliaji John Rafael Bocco, ameshindwa kujumuika na wenzake kwenye safari, kufuatia kuwa majeruhi. Hamis Abdallah naye amesalia kutokana na matatizo ya kiafya.

Mbali na Bocco, wachezaji wengine walioachwa ni Thomas Ulimwengu na Farid Mussa, ambao imearifiwa wamekosa ruksa kutoka timu wanazozichezea.

Rashid Mandawa, Himid Mao na Shaaban Idd ni wachezaji walioongezwa na Kocha Mkuu, Salum Mayanga katika kikosi kilixhoondoka nchini leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic