March 19, 2018



Na George Mganga

Rais wa klabu ya Township Rollers,  Walter Kgabung, amewazawadia wachezaji wa kikosi cha kwanza kiasi cha dola za kimarekani USD 2500 kama bonazi kwa kila mmoja.

Kwa mujibu wa Sports Extra, Clouds FM, imeripoti kuwa fedha hizo zimetolewa kama njia ya kuongeza hamasa kwa wachezaji wa kikosi hicho, kufuatia kuindoa Yanga katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Jumamosi ya wiki iliyopita.

Rollers walifanikiwa kuindosha Yanga na kuingia hatua ya 16 bora kwa mara ya kwanza kwenye mashindano hayo.

Aidha, Kgabung ametoa pia bonasi ya USD 2000 kwa wachezaji wa akiba, na wale ambao hawakuwepo kikosini wakipokea USD 1500.

Kikosi hicho sasa kinasubiri timu ambayo itapangwa kucheza dhidi yake, baada ya droo inayotaraji kufanyika Machi 21 2018.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic