March 17, 2018




Na Mwandishi Wetu, Port Said
Kuhakikisha Simba inaona wako wanaoiunga mkono ugenini, wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Mji wa Cairo wanatarajia kuwasili hapa leo tayari kwenda uwanjani kuishangilia Simba.

Simba inaivaa Al Masry katika mechi ya Kombe la Shirikisho ikiwa ni mechi ya pili baada ya sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam.

Uongozi wa Simba umefanya juhudi kuandaa magari ambayo yatawabeba wanafunzi hao Watanzania wanaosoma katika vyuo mbalimbali vikuu vya Cairo kuja hapa Port Said kuishangilia Simba.

Wanafunzi hao watakuja na kuondoka wakisafiri kwa zaidi ya saa tatu kuja hapa Port Said kuiongezea Simba nguvu.

Hapa Port Said hakuna chuo kikuu chenye Watanzania ndiyo maana Simba wakafanya utaratibu kuwasaidia wanafunzi hao kufika ili kuungana nayo hapa wakati wa mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic