March 11, 2018


Kikosi cha Yanga kitafanya mazoezi ya mwisho Jumapili ya leo kabla ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United.

Yanga itashuka Uwanja wa Taifa kesho ikiwa na utofauti wa alama tatu pekee kuwa sawa na Simba anayeongoza ligi hivi sasa.

Mchezo huo utakuwa wa mwisho kwenye ligi, kabla ya safari kuelekea Gaborone kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Township Rollers FC.

Katika mchezo wa ligi uliopita, Yanga iliipa kichapo kikali Kagera Sugar cha mabao matatu kwa sifuri.

3 COMMENTS:

  1. Hao Stand United walipokutana na Simba aliepungukiwa meno wakapata sare basi wakachonga sana kama vile walishinda game. Wathibitishe kesho tena kwa yanaga kama kweli wanaweza. SIMBA iliwakosa washambuliaji wake wawili tegemeo roho yao ya ufangaji lakini majigambo ya stand United baada kutoka sare na Simba kwa kweli yalitia kichefu chefu.

    ReplyDelete
  2. Mbona stand alipigwa 4-0 kwao, hiyo tatu ni ya lini tena

    ReplyDelete
  3. Kwa Dar walitoka sare ya ngapi ngapi si ilikuwa 3-3, wanafungwa wanarudisha, wanafungwa wanarudishwa, hukumbuki mdau?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic