Tiketi za mechi ya pili kati ya wenyeji Al Masry dhidi ya Simba, zimeanza kuuzwa lakini masharti yake ni kiboko.
Tiketi hizo zinauzwa na mashabiki watakaoingia wanatakiwa kujiandikisha na kila anayeomba tiketi lazima aandike taarifa zake muhimu, la sivyo hawezi kupata tiketi hata kama ana kibunda chake mkononi.
Mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kwa timu hizo iliisha kwa sare ya mabao 2-2 na sasa inasubiriwa ya marudiano.
Taarifa zinazotakiwa ni tarehe ya kuzaliwa, utaifa, kazi, enero analotokea, majirani zake, anuani, namba ya simu, anuani ya email, picha, namba ya kitambulisho cha utaifa kwa wale ambao ni miaka zaidi ya 18, lakini walio chini ya miaka 16 wataingiza taarifa kama hizo pamoja na vyeti vya kuzaliwa.
Atakayeorodhesha atakuwa amemaliza kujisajili na sasa kusubiri jibu la maombi yake ya tiketi.
Hii pia inatokana na hofu ya vurugu ambayo imekuwa ikijitokeza katika viwanja vya soka nchini Misri.
Wakati fulani katika mji wa Port Said waliwahi kufa watu zaidi ya watano kutokana na vurugu kubwa zilizotokea uwanjani.
Wachezaji wa Al Ahly akiwemo nyota Mohammed Abou Trika walikuwa ni kati ya watu walionusurika kuwawa katika vurugu hizo.








Almasry,hawa jamaa mashabiki wao hawafai. Wakorofi hasa na hii inatokana na asili ya wakaazi wake wa Port said kama wanavyojulikana wenyewe yaani Bousaid. Muulize Mmisri yeyote kuhusiana na waswahili hao wa Egypt na vurugu zao zilizoambatana na sifa ya ukaidi na ulaghai. Inasemekana neno Mswahili kwa maana ya mtu wa pwani pale ndio asili yake. Simba wanatakiwa kuwa na tahadhari kuhusiana na masuala ya usalama muda wote wakiwa kule. Kuanzia Malazi mpaka, chakula,usafiri mpaka kwenye vyumba vya kwenda kupumzika wakati wa mapumziko. Hawa jamaa wapo tayari kufanya lolote kuhakisha wanapata ushindi kwao.
ReplyDelete