March 15, 2018


Kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Al Masry SC dhidi ya Simba SC, Simba wamewasili salama nchini Misri Alhamis ya leo, Machi 15 2018.

Mapokezi ya Simba yamekuwa tofauti na wengi walivyotarajia kutokana na desturi ya Waarabu kufanya figisu ama mbinu ya kuwadhoofisha wapinzani wao, haswa kwa timu zinazotoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Kabla ilikuwa imezoeleka kuwa na vurugu nyingi na mambo mbalimbali yalikuwa uanasababisha kero.

Lakini safari hii mambo yamekuwa mazuri na hakuna figisu kwa kuwa Simba walijipanha vizuri na kufanya mambo yao wenyewe na hakukuwa na tatizo lolote.

Simba tayari iko katika mji wa Port Said ikiwa inaendelea na maandalizi yake vizuri kabisa.

Simba inafanya mazoezi muda ikiwa inatakiwa ishinde angalau bao 1-0 ili iweze kusonga mbele.

3 COMMENTS:

  1. tunawaombea afya njema na usalama kwa mungu wachezaji wote pamoja na viongozi mlio ambatana na team
    ya simba sc huko masri maombi yetu tuna waombea kila lenye kheri nanyi ili muweze kuibuka na matokeo mujarabu dhidi ya almasri..

    ReplyDelete
  2. Inshalla Mungu yupo nanyi na mtarejea nyumbani nyuso juu zenye kungara huku mkipokelewa kwa mapokezi ya aina yake Yaa Rab unatusikia waja wako

    ReplyDelete
  3. Kwa mfumo humo ambao wameondoka nao ni vema kulinda lango lao na kushambulia kwa kushukiza na kupata bao la mapema ili kuwachanganya waarabu hao. Kila la Kheri Simba kwenye mechi yenu ya kesho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic