BOCCO ATOA KAULI HII KUELEKEA MCHEZO WA SIMBA NA LIPULI, NI HAKUNA KULALA
Nahodha wa Simba, John Bocco, amesema mapambano yanaendelea katika michezo yote ijayo ya ligi kwa kuwa lengo lao kubwa ni kupata ubingwa.
Mchezaji huyo ambaye jana alifunga bao la kwanza wakati Simba ikikipa na Tanzania Prisons Uwanja wa Taifa, amesema mechi na Lipuli si ya kubeza.
Bocco ameeleza kuwa wanaijua Lipuli vizuri na watahitaji kupambana ili kupata matokeo waweze kutenegeza mazingira mazuri ya kubeba taji.
Wekundu hao wa Msimbazi walifanikiwa kuitandika Prisons mabao 2-0 jana na kufikisha alama 58 kileleni.
Simba itashuka Uwanja wa Samore Aprili 21 Jumamosi ya wiki ikiwa mgeni wa Lipuli kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Hongera sana BOCCO umeonyesha hekima na utawala bora kwa kuonyesha ushirikiano kwa wachezaji wenzako ili kuipatia simba sc mafanikio, mashabiki tunawatakia mafanikio kikosi chote cha simba sc muendelee na ushirikiano huo mpaka mwisho wa ligi na tuna matumaini makubwa kutoka kwenu kwa jitihada unazo onyesha kuhamasisha wachezaji wenzako ili simba sc iweze kuchukua ubingwa bila ya kupoteza mchezo...
ReplyDeleteHoja imeungwa mkono
DeleteNguvu moja iringa
ReplyDelete