April 2, 2018



Wakati kikosi cha Yanga kikiwa kinatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam leo, gumzo kubwa mitandaoni hivi sasa ni kuhusiana na Kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi.

Gumzo hilo limeanza mapema jana kufuatia kukosa mkwaju wa penati aliopiga na kupaa juu ya lango wakati wa hatua ya matuta.

Kiungo huyo alipaisha penati hiyo katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United katika Uwanja wa Namfua mjini Singida jana.

Kitendo cha kupaisha mpira huo juu ya lango kumewafanya mashabiki wa upande wa pili, Simba SC, kuanza kuchukulia kama sehemu ya utani.

Wapo wanaoandika kuwa mpira huo bado upo hewani kuelekea Morogoro, wengine wanataniana kwa kuhamasishana wavae kofia ngumu za pikipiki 'helmet' ili usije ukawapiga vichwani na kuumia. Yote hii ni desturi ya utani wa jadi kama ilivyozoeleka kwa Simba na Yanga.

Yanga iliondolewa na Singida United katika mashindano hayo kwa mikwaju minne dhidi ya miwili ya penati, na kuwafanya Singida wasonge mbele mpaka hatua ya nusu fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic