April 4, 2018




Mdau maarufu wa michezo nchini hasa soka, Hassan Hassanoo amesema amejipumzisha na masuala ya soka kwa muda.

Hassanoo ambaye amewahi kushika nafasi za juu katika klabu za Simba tena kwa mafanikio, amesema kwa sasa hajishughulishi na wala hayuko kwenye uongozi wowote.

“Nimesikia wanasema niko kwenye kamati namwaga mamilioni. Kweli kabisa mimi nimepumzika na mambo ya mpira na sasa nafuatilia kama mashabiki wengine.

“Siko katika uongozi wowote, siko katika kamati yoyote na wala siwezi kumwaga mamilioni kama ulivyosikia,” alisema Hassanoo.

Hassanoo aliyekuwa na sifa ya upambanaji wakati kikosi cha Simba kilipokuwa katika hali mbaya ya kifedha amesema hajakaa vizuri kama anavyotaka na badala yake sasa amejikita zaidi katika masuala ya kifamilia.


“Tokea wakati huo nimekuwa mtazamaji tu, si kiongozi,” alisisitiza.

2 COMMENTS:

  1. Nimeona Kwamba Hassanol hayupo kwenye Uongozi lakini nijuavyo Mimi yeye ni MWe Mwenyekiti wa FA MKOA WA PWANI

    ReplyDelete
  2. Labda huo siyo uongozi jamani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic