April 14, 2018


Na George Mganga

Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa aliwahi kuharibiwa mipango ya kujiunga na Yanga ili kuchukua nafasi ya ukocha wakati Abbas Tarimba akiwa ni mmoja wa viongozi ndani ya timu hiyo.

Julio ameeleza kuwa aliwahi kufanyiwa umafia na baadhi ya watu ambao walikuwa hawampi nafasi ya kupata nafasi hiyo.

"Niliwahi kupata nafasi Yanga ili niwe Kocha, lakini kuna baadhi ya watu waliokuwa hawana nia njema wakati Abbas Tarimba akiwa kiongozi waliniharibia mipango" amesema Julio.

Mbali na hilo, Kocha Julio amesema yupo tayari kuinoa Yanga ambayo imeondokewa na Kocha wake Mkuu, George Lwandamina, aliyerejea kujiunga na timu yake ya zamani, Zesco United, nchini Zambia.

kwa mujibu wa E Sports kutoka EFM, Julio anaamini anaweza kuifundisha Yanga kutokana na uzoefu alionao ndani ya soka la Tanzania sababu akieleza ameshafundisha baadhi ya timu hapa nchini.

"Nipo tayari kufundisha kama watakubaliana namimi, nina uzoefu wa kutosha katika kazi hii" amesema.
 

Yanga hivi inajiandaa na safari ya kesho kuelekea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili ambao ni wa marudiano dhidi ya Wolaitta Dicha FC.

4 COMMENTS:

  1. Julio, Dodoma FC umefikia wapi?

    ReplyDelete
  2. Una roho ngumu Julio

    ReplyDelete
  3. Kweli mchukueni na atakufikisheni mbale kama alivowafikisha Simba. Ni kocha mwenye uwezo

    ReplyDelete
  4. Anakuja kuiba siri za yanga awape cmba fisi kwenye zizi LA kondoo?mnataka ahujumu yanga wafungwe 20?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic