April 28, 2018



Washambuliaji wa klabu ya Simba, Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi na John Bocco, wamepewa nafasi kubwa na mashabiki wa timu hiyo kuonesha makali watakapokutana na Yanga Jumapili ya wiki hii.

Asilimia kubwa ya mashabiki wengi wamempa nafasi Kichuya ya kucheka na nyavu kutokana na rekodi yake hivi karibuni inaonesha amekuwa akiifunga Yanga kila wanapokutana.

Tambo hizo za Wanasimba zimeendelea haswa vijiweni na mitandaoni huku wengi wakijiamini kuwa wako vizuri msimu huu ukilinganisha na wapinzani wao.

Simba wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mechi hii itakayopigwa Jumapili ya kesho kutokana na kikosi kipana ilichonacho na rekodi yake ambapo mpaka sasa haijapoteza mchezo hata mmoja.

Mara nyingi timu hizi zinapokutana huoneshana upinzani mkali Uwanjani bila kujalisha timu moja iko vizuri na nyingine haiko vizuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic