MKONGOMANI WA YANGA KUANDIKA HISTORIA HII
Na George Mganga
Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera, amekiongoza kikosi cha Yanga kujifua wakati kikiwa mjini Morogoro ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kuondoka kwa Mzambia, George Lwandamina.
Zahera anaenda kuweka historia ya kuiongoza Yanga katika mechi dhidi ya watani wa jadi endapo atakuwa kwenye benchi la ufundi.
Historia hiyo itakuwa kubwa kwake na kipimo kizuri kitakachotoa taswira yake na Yanga baada ya mchezo kumalizika.
Mkongo huyo ameasili nchini wakati Yanga ikiwa katika wakati mgumu hivi sasa haswa kuyumba kiuchumi tofauti na msimu mmoja uliopita.
Taarifa zinaelezwa kuwa bado Kocha huyo hajasaini mkataba na Yanga japo tayari ameshaanza kazi rasmi kutokana na uongozi huo haujaweka wazi kuhusiana na mkataba ndani ya mabingwa hao wa ligi waliotwaa taji hilo mara 27.
0 COMMENTS:
Post a Comment