April 19, 2018



Manchester United imeendelea kukatia kiti cha nafasi ya pili katika ligi kuu England baada ya kuicharaza Bournemouth mabao 2-0 Jumatatu ya jana.

Smalling na Lukaku walifunga mabao hayo na kuifanya United ifikishe jumla ya alama 74 ikiwa imechezea michezo 34 msimu huu.

Ushindi unazidi kuzima ndoto za Liverpool kukamata nafasi ya pili kutokana na kipigo walichotoa leo kwa Bournemouth kilichosababisha kuongeza alama tatu muhimu.

Liverpool yenyewe ipo katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 70 huku ikiwa imecheza michezo 34 pia.

United imepooza machungu baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya West Brom katika mchezo uliopita.

1 COMMENTS:

  1. Sio Newcastle ni Westbrom Albion....embu kabla hujapublish kwny public fanyeni Editorial

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic