April 3, 2018



Na George Mganga

Timu ya Njombe Mji FC ina kibarua kigumu cha mchezo wa ligi dhidi ya Simba iliyo na njaa ya kuukosa ubingwa kwa takribani miaka mitano.

Njombe Mji itahitaji kupata matokeo kwenye mchezo wa leo ili kujiwekea mazingira ya kuepuka kushuka daraja ambapo mpaka sasa ina alama 18 ikicheza jumla ya michezo 22 huku ikishika nafasi ya 15 kwenye ligi.

Kikosi hicho kinakutana na Simba iliyoweka utofauti wa pointi 28 na Njombe Mji ambayo inapambania kuepuka kushuka daraja.

Kama Njombe itapoteza mtangane wa leo itazidi kuporomoka zaidi kwenda chini na kujitengenezea mazingira magumu kusalia kwenye ligi msimu huu.

Njombe pia inaingia kucheza mechi hii baada ya kuondoshwa na Stand United kwenye Kombe la Shirikisho pia ikikumbuka kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Simba katika mzunguko wa kwanza wa ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic