April 28, 2018



Kueleka mechi ya watani wa jadi iliyo na hisia kubwa kwa mashabiki wengi hapa nchini, kumekuwa na maoni tofauti ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya wadau wa soka.

Kila mdau amekuwa akizungumza la kwake kutokana na asili ya timu hizo zinapokaribia kukutana huwa kuna majigambo mengi haswa vijiweni na kwenye mitandao.

Kocha wa zamani wa Simba, Jackson Mayanja, yeye amesema kuwa mechi hiyo haitakuwa na presha kwa Simba kutokana na timu hiyo kuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi.

Mayanja ameeleza Simba hata kama akipoteza mchezo huo hautakuwa na madhara kwake kutokana na utofauti wa alama ilizo nazo dhidi ya Yanga.

Kocha huyo ambaye aliwahi kuwa Msaidizi wa Mcameroon, Joseph Omog, anaamini kuwa Simba inaingia kucheza mchezo huo ikiwa ina faida ya kuwa na alama nyingi dhidi ya Yanga, japo akisema yoyote atakayekuwa amejipanga vema atapata matokeo.

Simba mpaka sasa ina alama 59 juu ya kilele cha msimamo wa ligi, huku Yanga ikiwa na pointi 48.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic