April 28, 2018



Na George Mganga

Ni siku moja pekee ambayo ni leo Jumamosi imesalia kuelekea mechi kubwa ya vigogo wa katika soka la Tanzania Simba na Yanga watakaokutana kwenye Uwanja wa Taifa kesho Jumapili.


Simba na Yanga zinakutana kwenye mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara zikiwa na kumbukumbu ya kwenda sare ya bao 1-1 kwenye mechi ya raundi ya kwanza.


Yanga inaenda kuchuana na Simba ikiwa mgeni huku ikiwa haina uhakika wa kuwatuma baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa hawana hali nzuri kiafya tangu msimu huu wa 2017/18 uanze.


Wachezaji hao ni Donald Ngoma na Amis Tambwe ambao wamekosekana kwenye mechi lukuki kutokana na kuandamwa na majeruhi.


Ingawa uongozi wa Yanga umekuwa ukitangaza kuwa wachezaji hao kuwa wako fiti kila inapotokea wanakuwa na mechi, wamekuwa wakishindwa kuonekana Uwanjani sababu ya majeruhi kuwaandama.


Mbali na wawili hao, Ibrahim Ajibu, Andrew Vincent na Kelvin Yondani ndiyo waliorejea kikosini baada ya kupatwa na majeruhi siku kadhaa zilizopita.


Urejeo wa wachezaji hao unaleta manufaa kwa kikosi cha Yanga ambacho kimetawaliwa na vijana wengi kwa msimu huu baada ya wakongwe baadhi kuonekana kwa nadra Uwanjani kwa sababu tajwa hapo juu.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic