April 24, 2018






Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga wameikatia rufaa Mbeya City.

Yanga wameikatia rufaa Mbeya City baada ya mchezo wao uliopita kuibuka kituko cha wenyeji City kucheza 11 wakati tayari mchezaji mmoja alishalambwa kadi nyekundu.

Taarifa zinaeleza tayari Yanga imewasilisha rufaa yake katika kamati ya saa 72 ya TFF.

Mkanganyiko huo ulitokea katika dakika za nyongeza wakati timu hizo zikimalizia muda.
Mechi hiyo iliisha kwa sare ya bao 1-1, Mbeya City wakisawazisha dakika za lala salama.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ndiye alikuwa wa kwanza kuamsha madai hayo akionyesha kwamba City hawakuwa wamepungua.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic