April 4, 2018



Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Afisa Habari wake, Dismas Ten, umewaomba mashabiki na wanachama wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha FC, Jumamosi hii.

Yanga itakuwa ina kibarua hicho cha mkondo wa kwanza baada ya kuondoshwa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Ten amewaomba mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi ili kutia hamasa kwa wachezaji waweze kuwa na ari pamoja na morali ya kujitoa uwanjani.

Kuelekea mchezo huo, tayari viiingilio vilishatajwa ambapo kiingilio cha chini kabisa kwa mzunguko kitakuwa ni shilingi 3000 pekee.

Viingilio vingine ni shilingi 15,000 kwa VIP A, 10,000 kwa VIP B na C huku mzunguko ikiwa ni 3000 pekee.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic