May 4, 2018

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho ana hamu ya kumsajili winga wa Ajax Justin Kluivert 18, mwana wa mchezaji wa zamani wa Uholanzi Patrick Kluivert. (Mirror)
Everton wanataka kumuajiri aliyekuwa mkufunzi wa Watford Marco Silva ili kuchukua mahala pake Sam Allardyce. (Goal)
Bayern Munich itawasilisha ombi la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 24, iwapo watampoteza mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 29, mwisho wa msimu huu. (Bild, via Sun)
Arsenal imeibwaga Bayern Munich katika usajili wa beki kinda wa Uturuki mwenye umri wa miaka 21 Caglar Soyuncu, ambaye anaichezea klabu ya Freiburg nchini Ujerumani Bundesliga . (Evening Standard)
Crystal Palace inatarajiwa kufanya mazungumzo ya kandarasi mpya na kiungo wa kati wa Ufaransa Yohan Cabaye, 32, na beki wa Uingereza Joel Ward, 28, wiki ijayo ili kuweka wazi hatma yao katika klabu hiyo.. (Guardian)

Aston Villa itajaribu kumnunua kiungo wa kati wa West Brom Gareth Barry, 37, katika klabu hiyo iwapo watapandishwa daraja kutoka ligi ya mabingwa nchini Uingereza hadi ile ya premia. (Mirror)
Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV