ALIYEPINGA MABADILIKO SIMBA AKANUSHA KUONDOSHWA BMT, AMEFUNGUKA NAMNA HII
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohamed Kiganja, amekanusha taarifa zilizoenea kuwa ameondolewa kwenye baraza hilo.
Tangu jana kumekuwa na taarifa zinazoeleza kuwa Kiganja ameondola kwenye nafasi hiyo huku ikielezwa kuwa atapangiwa majukumu mengine ya kazi.
Kufuatia uwepo wa taarifa hizo, Kiganja amesema kuwa hajapokea barua rasmi ya kuondolewa kwenye kiti chake hivyo hawezi akakiri kama ameondoshwa na badala yake anasubiri barua rasmi kutoka kwa mabosi wake.
Kiganja aliteuliwa kushika nafasi hiyo na aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mh. Moses Nape Nnauye mwaka 2016.
Kiganja alijizolea umaarufu mkubwa kufuatia kauli zake zilizokuwa zikipinga mabadiliko ya mfumo wa kisasa wa uendeshwaji wa klabu za soka nchini, haswa Simba wakati wakianza mchakato huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment