May 18, 2018


Kocha Mtarajiwa wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera, ameondoka nchini kuelekea kwao Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya taifa.

Zahera ambaye ni Kocha Msaidizi wa Congo ameondoka huku Yanga ikiwa inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.

Kocha huyo bado hajasaini mkataba wa kuitumikia Yanga mpaka sasa na taarifa zinaelezwa kuwa bado wapo kwenye mazungumzo ya kumalizana naye taratibu.

Shadrack Nsajigwa pamoja na Noel Mwandila ndiyo wamekabidhiwa majukumu ya kuinoa Yanga ambayo vilevile inashiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Haijaelezwa Zahera atarejea lini lakini ameondoka nchini huku akiwa amewaaga viongozi wa Yanga ili kupata nafasi ya kwenda kutimiza majukumu ya Congo ambayo inajiandaa na mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika.

5 COMMENTS:

  1. Au nae ndio keshaingia mitini? Ikiwa ni kweli msikanushe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama hajaingia mitini lazima atakuwa amefuata mitishamba kama yule mchezaji wao nanhii ambaye wao humuita eti ni 'nyota'.

      Delete
  2. Si bure anaondoka wakayi huu ambao yanga in majukumu makuu. Kweli huyu keshaona kubaki yanga kutamgharimu na hakuna zuri la kutegemea

    ReplyDelete
  3. Sifikirii kama atarudi.Ameona bora ajitenge mapema kabla hajatengwa na asike akawa akingojea mishara kama ilivo kwa wachezaji

    ReplyDelete
  4. TUMENI PICHA ZAKE TUMNONE WAKATI AKIONDOKA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic