May 31, 2018


Kikosi cha timu ya taifa ya England kimeanza kujifua kwa kasi kubwa tayari kwa michuano ya Kombe la Dunia nchini Russia.

England inajifua kwa nguvu chini ya Kocha Garreth Southgate ambaye amepania kufanya mabadiliko makubwa. Kocha huyo anaelezwa sasa anataka kutumia mbinu za Kocha wa Man City, Pep Guardiola kwa ajili ya kuhakikisha kikosi chake kinafanya vema.

England itaanza michuano hiyo Juni kwa kupambana na wenyeji Russia ambao nao wamepania ile mbaya kufika mbali na kuushangaza ulimwengu.

Pamoja na kelele nyingi, England imekuwa ikiondolewa mapema katika michuano hiyo, lakini Southgate anaamini safari hii Russia mambo yatakuwa tofauti.











0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic