May 15, 2018



Katika kuhakikisha wanaongeza hamasa ya timu kuelekea mechi ya pili ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, mabosi wa Yanga walivamia mazoezi ya timu hiyo na kumwaga noti kwa wachezaji.

Yanga keshokutwa Juma­tano inatarajiwa kuwakari­bisha wapinzani wao Rayon Sports ya Rwandakatika mchezo huo wa makundi utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga tayari imepoteza mchezo wa kwanza katika kundi lao kwa kufungwa na USM Alger ya Algeriakwa kufungwa ugenini mabao 4-0.

Kwa mujibu wa gazeti la Champi­oni Jumatatu, limeeleza kuwa mabosi hao walifika katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam yakiongozwa na Mkongoman, Zahera Mwinyi.

Mtoa taarifa huyo al­isema mara baada ya kufika mazoezini, mabosi hao walionekana kufuatilia kwa makini na baada ya kumalizika walipata nafasi ya kuzungumza na viongozi, benchi na kikubwa kuwapa hamasa ya mchezo ujao dhidi ya Rayon na badaye kila mchezaji na kiongozi wa benchi la ufundi alipewa shilingi 50,000.

“Leo tulipata ugenini wa ghafla wa viongozi kutoka kamati ya mashindano wakiongozwa na mwenyekiti wake Nyika (Hussein), Luku­mayi (Samuel) na kiongozi mmoja jina lake siri ambaye yeye ndiye aliyetoa fedha hizo.

“Fedha hizo zilitolewa baada ya mazoezi kumal­izika na viongozi hao kuzun­gumza machache, kikubwa wamesisitiza umuhimu wa mechi licha ya timu kukabil­iwa na matatizo ya kifedha,” alisema mtoa taarifa huyo.

Aidha, Zahera alisema: “Ninafurahi kuo­na hamasa kubwa ikitolewa kwa wachezaji wangu katika kuelekea mechi na Rayon.

“Kama nilivyokwambia awali, bado baadhi ya wachezaji wameonekana kuweka mgomo kutokana na madai yao ya misha­hara, lakini nafarijika kuwaona wengine wakifika mazoezini.”

2 COMMENTS:

  1. Lakini uongozi.ulikanusha kuwrpo mgomo wa wachezaji.kudai mishahara.yao lakini kocha mwenyewe kayataja hayo, sasa basi nani mkweli

    ReplyDelete
  2. Sitafurahia posho nitafurahia kuona mishahara. Posho si deni ila mshahara ni deni. Viongozi au sijui mabosi wanachotakiwa kukijua ni kwamba wachezaji wanadai mishahara na si posho. wapewe stahiki zao alafu tuone kama watagoma..Ukiwanyima posho hawawezi kugoma ila ukiwanyima mishahara ni lazima wagome. Tunaomba wachezaji walipwe mishahara na si posho. Kwanini Mkwasa ambae ndio mtendaji mkuu anashindwa kuweka wazi haya mambo?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic