May 18, 2018


Na George Mganga

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka mashabiki wa Simba kutokuwa na wasiwasi juu ya usalama wa kesho katika mechi ya Simba dhidi ya Kagera Sugar itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Ofisi zake zilizopo Ilala, Boma jijini Dar, Makonda ameeleza ulinzi utakuwa wa hali ya juu hivyo ni vema mashabiki wakaenda kwa wingi.

Mbali na ulinzi, Makonda ameeleza kitendo cha Kombe la Bingwa wa Ligi Kuu msimu huu ambaye ni Simba kubakia Dar es Salaam ni faraja kubwa kwake akiwa kama Mkuu wa Mkoa.

Vilevile Makonda amesema uwepo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli atakayewakabidhi Simba kombe ni jambo kubwa kwakuwa hajawahi kuhudhuria mechi yoyote ile ya ligi.

Mkuu huyo wa mkoa hajawasahau watani zake wa jadi Yanga kwa kuwakaribisha katika mechi hiyo itakayoanza majira ya saa 8 na robo mchana kesho Jumamosi.

5 COMMENTS:

  1. Jamani naona mapenzi juu ya Simba yanazidi marudufu. Mungu azidi kuibariki

    ReplyDelete
  2. Huyu shetani ndiye aliyeimaliza yanga kwa kumtesa mfadhili wa Yanga Manji kumbe lengo lake lilikuwa ni kuchukua ubingwa kirahisi. Huna maana bashite mkubwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga walitulia, sindano ikaingia ndaaani kabisa, ... na sasa dawa inapenyeza tartiiiiib ...

      Maaaskiini Yaangaaaa!!!

      Ushindi ni uwanjaani mkuu - yule mhuni Manji alikuwa akiisaidia Mayebo kutwaa ubingwa nje ya uwanja. Ona sasa, mkiaa sawa mnatwangwa 4G, ... mkigeuka 0-0 na vibonde RAYON Sport.

      Go, Makonda - Go! Simamia haki kila pahala - hata michezoni pia. Mikono ya Tambwe na rufani za Kagera ndizo ziliipa ubingwa na uwakilishi feki hawa Mayebo!

      Makonda hoyeeee!!
      Magufuli Hoyeeeeee!!!
      Michezoo juuuuuuuu!!
      '... ndiyoo - juu, juuu juuuzaidiii ----- kaaaziiiiii!

      Delete
    2. Yanga walitulia, sindano ikaingia ndaaani kabisa, ... na sasa dawa inapenyeza tartiiiiib ...

      Maaaskiini Yaangaaaa!!!

      Ushindi ni uwanjaani mkuu - yule mhuni Manji alikuwa akiisaidia Mayebo kutwaa ubingwa nje ya uwanja. Ona sasa, mkikaa sawa mnatwangwa 4G, ... mkigeuka 0-0 na vibonde RAYON Sport. Sasa subirini kupaswapaswa (sio kupapaswa) na wale wajeeshjeesh!!

      Go, Makonda - Go! Simamia haki kila pahala - hata michezoni pia. Mikono ya Tambwe na rufani za Kagera ndizo ziliipa ubingwa na uwakilishi feki hawa Mayebo! Miaka miwili mfululizoo!

      Makonda hoyeeee!!
      Magufuli Hoyeeeeee!!!
      Michezoo juuuuuuuu!!
      '... ndiyoo - juu, juuu juuu zaidiii ----- kaaaziiiiii!

      WanaSimba tumiminike uwanjani mpaka bata na kunguru wote washangaeeee!!

      Delete
  3. Jamani kuweka maneno sawa aliemfanyia figisu Manji sio Makonda ni Mzee Akili Mali. Na aliemtia pirika Manji kutokana na vitendo vyake vya kihalifu sie Makonda bali ni Mwigulu Mchemba kama kamanda mkuu wa kuzuia uhalifu Tanzania. Yanga wapo Salama bila ya Manji cha kufanya kwa yanga na wanayanga ni kutafuta viongozi wapya wasiotumia madawa ya kulevya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic