May 31, 2018


Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara, amefunguka kwa kueleza kuwa anatamani wakutane na Yanga kwenye michuano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya.

Timu zote mbili zinaondoka asubuhi ya leo kuelekea Nakuru kupitia Nairobi kwa ajili ya mashindano hayo yanayoanza kurindima Juni 3 jijini humo.

Manara ametamba kuwa anatamani wakutane na Yanga ili waweze kuwaonesha namna walivyojipanga na akijigamba kuwa ni lazima wawafunge.

Simba wanaenda kushiriki mashindano hayo wakiwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara msimu uliomalizika (2017/18) ambapo walifanikiwa kuwa mabingwa.

Mbali na watani hao wa jadi, klabu za Singida United na JKU ya Zanzibar nazo zitasafiri kuelekea Kenya kushiriki michuano hiyo kwakuwa zipo chini ya udhamini wa kampuni hiyo ya bahati nasibu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic