May 18, 2018


Na George Mganga

Mdhamini wa zamani Barala la klabu ya Simba, Hamis Kilomoni, ameshukuru na kuupokea kwa mikono miwili mwitikio wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, kuhudhuria mchezo wa Simba na Kagera.

Simba itakuwa inacheza na Kagera katika Uwanja wa Taifa, mchezo ambao utaenda sambamba na hafla ya kuwakabidhi Simba kombe la ligi ambalo atalikabidhi Rais Magufuli.

Licha ya kufurahia ujio wa Magufuli ambaye atakuwa mgeni rasmi, Kilomoni amesema kuwa yeye bado ni mzee wa Baraza la Wadhamini wa Simba mpaka sasa, huku akiwaomba wanachama na mashabiki wajitokeze kwa wingi kesho Uwanjani.

Ikumbukwe Kilomoni alisimamishwa uanachama katika Mkutano wa Mabadiliko Simba uliofanyika mwaka jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa JK Nyerere uliopo Ocean Road, Posta.

Kilomoni ameenda mbali na kueleza kwa kusema kuwa, yeyote atakayejitokeza na kuleta ubaguzi ndani ya Simba, basi atakuwa hayuko pamoja na Simba yenyewe.

Ameongeza kwa kusema Simba imefikia hapa kutokana na umoja ilionao na hatimaye imefanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Bara msimu huu.


2 COMMENTS:

  1. Na kuna haja gani ya kumleta huyu mchochezi hapa? Ukisambaza matamshi ya kichochezi ya mtu mwengine na wewe mchochezi vile vile,Waandishi wanapaswa kuwa makini. Ubaguzi gani anaouzungumzia huyu mzee? Kweli anaijua tafsiri halisi ya neno ubaguzi? Kama ni ubaguzi yeye ni mbaguzi namba moja na inabidi atubu na kuomba radhi Watanzania na wanasimba. Kama SIMBA wangemuendekeza na kumlea lea huyu mzee basi hali ingekuwa mbaya kuliko inayowakuta Yanga hivi sasa. Yeye mzee kama anafurahia ubingwa muache afurahie lakini huu si wakati wa kuleta choko choko Simba ni wakati wa kusonga mbele kimaendeleo.

    ReplyDelete
  2. Kashindwa na fitina zake kwahivo anaogopa asitengwe na Simba iayoyotononoka kwa nguvu ambapo wajanja na wanafiki wanapikiwa jungu lao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic