May 4, 2018



Baada ya kuwakosa watani zake wa jadi, Yanga, kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima inaelezwa tayari amesharejea nchini kujiunga na klabu yake.

Niyonzima alisafiri wiki iliyopita kuelekea kwao Kigali, Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria msiba wa dada yake aliyefariki baada ya kuumwa.

Niyonzima amerejea huku Simba ikiwa na nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi, ambapo mpaka sasa imejikusanyia jumla ya alama 62.

Simba inahitaji kushinda mechi moja pekee na kwenda sare ama suluhu katika michezo ijayo ya ligi ili iweze kufikisha jumla ya alama 67 ambazo hazitoweza kufikiwa na timu yoyote ile.

Kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi yake katika Uwanja wa Bocco Veterani kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Jumapili ya wiki hii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic