May 11, 2018



Na George Mganga

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amesema kuwa alijua mapema kama Simba itautwaa ubingwa wa ligi msimu huu.

Rage ambaye aliwahi kuingozo Simba kabla ya uongozi wa Evans Aveva kuingia madarakani, amefurahia Simba kutwaa taji la ligi ambalo wekundu hao wa Msimbazi hakulipata kwa takribani misimu mitano.

Rage ameeleza kuwa Simba inafukuziwa na SMG na kimyakimya kama mwizi, kauli ambayo ilitolewa na watani zao wa jadi, Yanga.

Yote kwa yote Rage amewashukuru wanachama na mashabiki wa Simba kwa ujumla kutokana na kuonesha ile kauli mbiu yao ya Simba Nguvu Moja akiamini ndiyo nguzo kuu iliyowasaidia kupata ubingwa.

Kikosi cha Simba kitakuwa kinashuka dimbani Uwanja wa Namfua kesho Jumamosi kukamilisha ratiba ya ligi kwa kucheza na Singida United katika Uwanja wa Namfua mjini Singida.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic