May 4, 2018Kikosi cha Ruvu Shooting kimelazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Mabatini huko Mlandizi.

Bao pekee la mapema zaidi msimu huu kwa Mwadui FC limefungwa na Abdallah Seseme katika sekunde ya 12 mnamo dakika ya kwanza. Bao lilidumu kwa dakika 45 za kwanza huku ubao ukisomeka kuwa 1-0.

Ruvu Shooting ambao ilikuwa kidogo leo wakubali kupapaswa, walisawazisha kupitia kwa Fully Maganga katika dakika za mwisho mwa mchezo.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Ruvu 1 na Mwadui FC 1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV