May 4, 2018Mabingwa wa soka nchini Yanga, wametua salama nchini Algeria tayari kuivaa USM Alger, keshokutwa.

Yanga iko nchini humo tayari kuwavaa vigogo hao katika mechi yao ya kwanza ya hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Kikosi hicho mjini Algeri kimepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Omar Yusuph Mzee.

Balozi huyo ambaye ni mwanamichezo, aliwapokea na kuwasindikiza hadi hotelini na kesho, Yanga watafanya maandalizi yao ya mwisho kabla ya mechi hiyo ya keshokutwa.
2 COMMENTS:

  1. HAPA KUNA KITU NYUMA YA PAZIA KUNA WADHAMINI WATATU WAKUBWA SASA KWANINI WANASHINDWA KULIPA MISHAHARA? WACHEZAJI MBONA HAWAPONI MAJERAHA? KWENYE MECHI MUHIMU KWANINI NDIPO UDHURU UNAIBUKA? WALE WENYE FEDHA WAKO WAPI YANGA? NIDHAMU YA WACHEZAJI MBONA IKO CHINI NANI ANAHUSIKA NA HILI? KIBALI CHA KOCHA KWANINI MCHAKATO UMECHUKUA MUDA? USHAURI YANGA IJITOE MASHINDANONI KULIKO KUTULETEA AIBU....HIVI TUKISIKIA WANAFUNGWA 8-0 KUNA KULAUMU? HII NI HATARI SANAAA....HIVI WAPENZI WA YANGA WENGI WANAUGUA NA KUFEDHEHEKA MWAKA HUU.....KWENYE MSAFARA VIONGOZI NI WENGI 11 NA TIMU ILIYOENDA NA YOSSO 17....MNAFANYA MASIHARA NYIE MNAENDA KUCHEZA NA MABINGWA WA ALGERIA WENYE MAANDALIZI NA MASHABIKI WENYE NGUVU....MBONA KILIO TUNAKITAFUTA WATANZANIA JAMANI

    ReplyDelete
  2. Alimuradu yanga fujo na wala hakuna chakueleweka. Wachezaji wanagoma eti Ajibu anesthesia kupata mtoto wakati wowote wachezaji wanagoma wao wanawakingia kifua.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV