May 13, 2018



Mshambuliaji Mbwana Samatta ameendelea kurejea kwenye fomu yake baada ya kuifungia timu yake ya KRC Genk mabao mawili katika ushindi wa 4-1.

Genk imeitwanga Sporting Charleroi kwa mabao 4-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Ubelgiji, leo.

Samatta ambaye alikuwa majeruhi, amekuwa akirejea taratibu na tayari alishafunga bao katika mechi iliyopita.

Katika mechi ya leo, Samatta alianza kufunga bao katika dakika ya 24, bao lake la pili lilikuwa katika dakika ya 61 likiwa la tatu katika mchezo huo kwa upande wa Genk.

Bao la pili lilifungwa na Leandro Trossard katika dakika ya 44 na Ndongala ndiye alipigililia msumari wa mwisho wa Genk katika dakika ya 77.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic