SIMBA KUAMUA HATMA YA MAJIMAJI LIGI KUU BARA LEO
Kikosi cha Simba kinashuka dimbani kucheza na Majimaji mjini Songea katika mchezo wa kuhitimisha safari ya Ligi Kuu Bara msimu huu.
Simba ambao tayari ni mabingwa wa ligi msimu huu wataamua hatma ya Majimaji kama itaweza kuendelea kusalia kwenye ligi msimu ujao au kushuka.
Endapo matokeo ya mechi hiyo yatamalizika kwa Simba kuibuka na ushindi, safari ya Majimaji itakuwa imeishia hapo na itakuwa imeteremka rasmi mpaka daraja la kwanza.
Majimaji itapigania kupata alama tatu huku ikiomba dua zake kwa Stand United iweze kuifunga Ndanda ili ipate nafasi ya kusalia kwenye ligi.
Msimamo wa ligi unaonesha Ndanda ipo nafasi ya 14 ikiwa na alama 26 wakati Majimaji imeshika namba 15 ikiwa na alama zake 24.
Utofauti wa pointi hizo unaipasa Majimaji kushinda dhidi ya Simba ili kubaki kwenye ligi na endapo Ndanda itafungwa na Stand United. Lakini matokeo yakiwa kinyume, Ndanda atabaki huku Majimaji akiungana na Njombe Mji ambayo tayari imeshashuka daraja.
0 COMMENTS:
Post a Comment