May 18, 2018



Baada ya kushindwa kutamba dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa Jumatano ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, uongozi Yanga wasema bado una nafasi.

Katibu wa Mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa, ameeleza kuwa kushindwa kupata matokeo mpaka sasa kwenye michuano hakuwanyimi nafasi ya kufanya vizuri.

Mkwasa anaamini kuwa Yanga bado ina nafasi ya kupigania kufanya vizuri kutokana na mechi zilizosalia kwenye kundi lao ambalo wapo na USM Alger, Rayon Sports na Gor Mahia FC ya Kenya.

Yanga haijaweza kufikisha alama hata mbili mpaka sasa zaidi ya moja iliyopata juzi kufuatia suluhu dhidi ya Rayon.

Ratiba inaonesha Yanga itakuwa inawakaribisha Gor Mahia FC ambao wameenda suluhu na USM Alger huko Kenya juzi Jumatano, mechi ikitarajiwa kufanyika Juni 17 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic