May 18, 2018



Kikosi cha Yanga kimeondoka alfajiri ya leo jijini Dar es Salaam kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mechi ya ligi dhidi ya Mwadui FC.

Jumla ya wachezaji 20 pamoja na viongozi 8 wa timu hiyo wameondoka kuelekea mjini humo ambapo watacheza na Mwadui Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.

Yanga inaondoka ikiwa na rekodi mbaya ya kutoshinda mchezo hata mmoja tangu kuondoka kwa Kocha George Lwandamina aliyerejea kwao Zambia kuitumikia Zesco United.

Taarifa zinaeleza baadhi ya wachezaji ikiwemo Papy Tshishimbi na Donald Ngoma hawajaambatana na kikosi kuelekea Shinyanga kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Ikumbukwe Tshishimbi alisafiri kuelekea kwao Congo kupata matibabu ya mitishamba baada ya kuumia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaita Dicha SC.

2 COMMENTS:

  1. Ajib is not mentioned in the list if among players to conftont Mwadui.Are his outstanding salaries that made him boycott the team settled and same problems assured not repeatable or temporary fragile solution? We wish yanga best of luck

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic