ACHANA NA KAGERE, SIMBA YASHUSHA STRAIKA MWINGINE HATARI KUTOKA NIGERIA
Ukiachana na straika Meddie Kagere aliyetoka Gor Mahia FC kumalizanana mabosi wa Simba baada ya kutua jana nchini, wekundu hao wa Msimbazi wamemshusha mchezaji mwingine kutoka Nigeria, imeelezwa.
Ujio wa Kagere umeambataba na mshambuliaji mwingine kutoka Nigeria, Victor Patrick ambaye amekuja kufanyiwa majaribio na endapo atafuzu ataingia mkataba na klabu hiyo.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa Patrick amewasili kimyakimya nchini na kufichwa na matajiri hao wapya wa jiji la Dar es Salaam katika hotel moja kubwa jijini humo.
Simba wamezidi kuonesha jeuri ya fedha baada ya kumrejesha Pascal Wawa ambaye aliwahi kuichezea Azam FC.
Wakati huo kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani asubuhi ya leo kujiandaa na michuano ya KAGAME inayoanza Juni 29 2018.
Duh hapo ndo sielewi... yaani 'Straika hatari anakuja kufanya majaribio'!!! Ina maana klabu haijui kwamba ni straika hatari (ndo maana anafanya majaribio) ila mwandishi anajua ni straika hatari!!!
ReplyDeleteAu kwa kuwa anatoka Nigeria atakuwa (kwa mujibu wa Mwandishi) ni straika hatari!!!!
Mtusaidie basi kuandika habari za kina na utafiti kidogo... kwa mfano anatoka klabu gani, ni klabu ya daraja la ngapi, kafunga magoli mangapi n.k.
Jina hilo la Victor Patrick sijaliona kwenye rada za wachezaji hatari wa Nigeria. Ngoja tuje tumuone uwanjani labda kweli ni moto.
ReplyDeletekweli hajaonekana
Deletehapo kagere umechemsha.. tulikusaidia sana gor wakati haukua na club.. sasa tumekunoa ni simba umeenda.. kwani tabia za simba huzijui wewe? ni mchezaji mgani wa kigeni amekaa simba miaka mitatu?
ReplyDeleteKabisa mchezaji hatari hafanyiwi majaribio atafanyiwa vipimo vya afya. Huwezi kumfanyia majaribio Kagere? Kwanza Mchezaji mwenyewe kitendo cha kukubali kufanyiwa majaribio basi kesha muondolea hali ya kujiamini.
ReplyDeleteNa majaribio yenu muyafanye siri kwasababu majasusi wa simba hujibana pembeni na mtasitukia mkiwatumikia Simba, mara yukowapi? Unajibiwa kaonekana Msimbazi akizungumza na Manara
ReplyDelete