MSHAMBULIAJI HUYU KUTOKA FC LUPOPO ATUA YANGA KWA SIRI KUFANYA MAJARIBIO
Wakati Simba wakitamaba na ujio wa Meddie Kagere na Pascal Wawa hivi sasa ambao wapo kwenye mazungumzo na klabu hiyo, watani zao wa jadi Yanga tayari walikuwa wameshaleta straika kwa siri kutoka Congo, imeelezwa.
Ujio wa straika huyo anayejulikana kwa jina la Heritier Makambo, umetokana na Kocha wake Mku, Mwinyi Zahera ambaye alishuka naye juzi kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam.
Makambo ambaye alikuwa anaichezea FC Lupopo ya Congo, aliletwa kwa sirisiri na Zahera wakati akitokea nchini kwao kwa ajili ya mapumziko baada ya kurejea kwao na kutimiza moja ya majukumu ya kuwtafutia Yanga straika huyo.
Imeelezwa kuwa mchezaji huyo ataungana na Mbenini Marcelina Koukpou kwa ajili ya majaribio na kikosi cha Yanga mapema baada ya kambi maalum kuwawinda Gor Mahia FC kuanza wiki hii.
Yanga imekuwa ikiendesha harakati zake za usajili wa kimyakimya ili kutoibiwa wachezaji wake na baadhi ya timu ambazo zimekuwa zikiwafanyia umafia.
Kamati Maalum ya Ushauri na Mpito iliyopitishwa na Wanachama wa Yanga kupitia mkutano mkuu wa klabu uliofanyika hivi karibuni, umekuwa ukifanya harakati za usajili kwa siri nzito ili kutowapa chabo wapinzani.
great moves
ReplyDeleteYanga naipenda ila hali ya kiuchumi ni zaidi ya kifo
ReplyDeleteViongozi watangaze tu harambee tuchangishane tupate pesa tusajili hata watoto wa daraja la kwanza tu! Tukiiga simba tutapasuka msamba
ReplyDelete