June 26, 2018


Na George Mganga

Beki mpya wa kulia wa klabu ya Azam, Nicholas Wadada, amewasili nchini majira ya mchana huu akitokea kwao Uganda kwa ajili ya kuitumikia timu yake mpya.

Wadada ambaye tayari ameshamalizana na kusaini mkataba, ametua rasmi Dar es Salaam tayari kwa mashindano ya KAGAME yanayotarajiwa kuanza Juni 29 2018 wiki hii.

Mchezaji huyo amekuja kuongeza makali ya safu ya ulinzi akisaidia na mkongwe, Aggrey Morrisi ambaye naye amesaini mkataba wa miaka miwili leo kuendelea kuichezea Azam.

Kuelekea michuano ya KAGAME, Azam itaanza kibarua chake ufunguzi wa mashindano dhidi ya Kator FC Juni 29 kwenye Uwanja wake wa nyumbani, Chamazi Complex.

Ikumbukwe Azam ndiyo mabingwa watetezi wa kombe la KAGAME baada ya kulitwaa katika fainali ya kufana iliyochezwa Jumapili jioni Agosti 2 katika Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic