Klabu ya soka ya Azam imeanza vema kuutetea ubingwa wa michuano ya KAGAME kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kator FC ya Sudan Kusini.
Mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Chamanzi Complex ilishuhudiwa Azam wakijipatia mabao yao kupitia kwa Shaban Idd Chilunda aliyefunga katika dakika za 18 na 49.
Wakati huo klabu ya JKU kutoka Zanzibar imeshindwa kutamba dhidi ya Vipers SC ya Uganda baada ya kwenda sare ya 1-1.
Mechi nyingine inayotarajiwa kuanza punde usiku huu ni Singida United dhidi ya APR kutoka Rwanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment