SINGIDA UNITED YAANZA VEMA KAGAME, YAITWANGA APR 2-1 TAIFA
Klabu ya Singida United imeanza vizuri mashindano ya KAGAME baada ya kuitwanga APR kutoka Rwanda mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao ya Singida United yamewekwa kimiani na Habibu Kyombo pamoja na Tiber John waliosajiliwa na kikosi hicho baada ya msimu wa ligi 2017/18 kumalizika.
Ushindi huo umeleta matumaini kwa timu za Tanzania kuanza vema baada ya Azam nayo kuweza kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kator FC kutoka Sudan Kusini.
Katika mechi za ufunguzi leo, JKU ya Zanzibar ndiyo timu pekee kutoka Tanzania iliyoshindwa kung'ara kwa kulazimishwa sare ya 1-1 na Vipers SC ya Uganda.
Kesho Simba watafungua pazia lao rasmi kwa kucheza na Dakadaha ya Somalia, mchezo utakaoanza saa 8 kamili mchana.
0 COMMENTS:
Post a Comment