FELLAINI ASAINI MKATABA MPYA MANCHESTER UNITED
Kiungo wa Manchester United, Marouane Feallaino, ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kutumikia klabu hiyo.
Hapo awali ilikuwa inaelezwa kuwa Mbeligiji huyo anaweza akaondoka United lakini mambo yamekuwa tofauti na kiungo huyo ameweza kuongeza kandarasi ya miaka miwili.
Mkataba wa United na Fellaini sasa utamalizika mwaka 2020 baada ya kukubaliana na uongozi wa United ikiwemo hitaji la Kocha Jose Mourinho.
Fellain ameifungia United jumla ya mabao 20 katika michezo 156 ambayo ameichezea klabu hiyo.
Baada ya kusaini mkataba, Fellaini amesema anafurahia kuendelea kusalia United kutokana na furaha aliyonayo ndani ya timu hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment