June 1, 2018



Kiungo Himid Mao, ametua katika kikosi cha Petrojet ya Misri na ameamua kuwaaga Azam FC kwa ujumbe maalum.

Katika ujumbe wake mtandaoni, Himid ambaye hadi anaondoka alikuwa nahodha wa Azam FC, amewaomba radhi wenzake kama aliwakosea na kusema amewasamehe kama walimkosea.

Ameshukuru malezi bora aliyopata akiwa hapo na kusisitiza angependa kuendelea kujifunza.

Kiungo huyo anayetokea jijini Mwanza, Kanda ya Ziwa, aliomba kupewa nafasi akajaribu changamoto nyingine kisoka.

Uongozi wa Azam FC nao ukaamua kumruhusu kama mmoja wa wachezaji wake waliofanya kazi yao kwa weledi na juhudi kuu wakiwa Azam FC.

1 COMMENTS:

  1. Huyu mchezaji ni Muungwana. Mungu amjalie apate mafanikio zaidi. Wachezaji wetu wengine igeni mfano huu wa uungwana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic