June 1, 2018


Hakuna asiyemfahamu Mzee Akilimali kutokana na umaarufu wake ndani ya Klabu ya Yanga ambako amekuwa akivutana na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo huku wakidai kuwa ndiyo anakwambia maendeleo ya klabu.

Jina lake halisi ni Ibrahim Akilimali, huyu ni Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga ambaye amekuwa akitoa maneno ya shombo kwa wachezaji au hata viongozi wa timu hiyo anapoona hawafanyi vizuri.

Siyo kwamba haipendi Yanga bali huyu ni Yanga lialia Lakini wapenzi wa soka nchini wamekuwa wakijiuliza mambo kadhaa kuhusiana na mzee huyo ambaye haishiwi vituko kila kukicha.

Global TV Online imefanya mahojiano maalum kujua mambo kadhaa muhimu kuhusiana na Klabu ya Yanga.


3 COMMENTS:

  1. Huyu MUGABE wa Yanga anastahili kufanyiwa kama alivyofanyiwa mwenzake wa Zimbabwe.Ni wakati wa kufanya maamuzi muafaka ili kumuonesha kuwa wanachama,wapenzi na mashabiki wa Yanga wamechoshwa na futuhi zake.

    ReplyDelete
  2. Fikra za Mzee Akilimali kwa mara ya kwanza nimemuelewa kiukweli. Fikra zake zilikuwa kichwani mwangu. Yanga ni Taasisi bhana. Huwezi lia njaa kama unaongoza Yanga. Huwezi shindwa pata mkopo kama unaongoza taasisi kama yanga. Shida ni fikra duni za viongozi. Labda waseme hawawezi kukopesheka. Au waseme waoga wa kukopa.

    ReplyDelete
  3. Ama kweli. Akimili mali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic